Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mwandishi wa habari wa "Al-Sumaria" ameripoti kuwa mamia ya watu kutoka vikosi vya Kataib Hezbollah, Sayyid al-Shuhada na al-Nujaba waliandamana mbele ya “Daraja ya Al-Mu‘allaq” kuonesha mshikamano na Iran.
Alfajiri ya Ijumaa (13 Juni 2025), utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Iran, ambapo hadi sasa maeneo ya makazi ya raia, viwanda, na miundombinu ya nyuklia ikiwemo mitambo ya Natanz yamelengwa na kushambuliwa. Iran nayo ilijibu kwa kurusha ndege zisizo na rubani (drones), na kisha kufuatia na wimbi la makombora ya masafa marefu dhidi ya Israel.
Maoni yako